Skip to content

Latest commit

 

History

History
131 lines (76 loc) · 7.13 KB

README.sw.md

File metadata and controls

131 lines (76 loc) · 7.13 KB

Open Source Love License: MIT Open Source Helpers

Mchango wa kwanza

Ni vigumu. Mara zote ni vigumu kufanya kitu kwa mara ya kwanza. Hasa hasa kama unashirikiana na wengine, kufanya makosa sio jambo la kushangaza. Tulitaka kurahisisha namna ambavyo wachangiaji wapya wa mifumo ya wazi wanavyojifunza na kuchangia kwa mara ya kwanza.

Kusoma makala na kuangalia mafunzo ya video yaweza kusaidia, Lakini ni jambo lipi bora zaidi kuliko kufanya kwa vitendo katika mazingira ya kujifunzia? Mradi huu unalenga kutoa mwongozo na kurahisisha namna ambavyo wachangiaji wapya wanavyoweza kuchangia kwa mara ya kwanza. Ikiwa unataka kuchangia kwa mara ya kwanza , fuata hatua zifuatazo.

Kama haujazoea kutumia 'command line', [waweza kutumia GUI.](#Makala ya namna ya kutumia nyenzo nyingine)

fork this repository

Kama hauna git kwenye kompyuta yako, pakua.

Tengeneza nakala ya repository kwenye akaunti yako ya Github

'Fork' repository hii kwa kubonyeza kitufe kilichopo juu ya ukurasa huu Kwa kufanya hivyo nakala ya repository hii itatengenezwa kwenye akaunti yako.

Tengeneza nakala ya repository kwenye kompyuta yako

clone this repository

Sasa clone repository kwenye kompyuta yako. Nenda kwenye akaunti yako ya Github bonyeza kitufe kilichoandikwa clone na baada ya hapo bonyeza kitufe kilichoandikwa copy to clipboard icon.

Fungua terminal kwenye kompyuta yako na weka command ifuatayo:

git clone "url uliyo nakili github"

url hiyo inapatikana kwenye hatua ya ku clone, hakikisha unaondoa fungua semi na funga semi.

copy URL to clipboard

Kwa mfano:

git clone https://github.com/jina-lako-unalotumia-Github/first-contributions.git

Kwa kufanya hivyo utakuwa umenakili first-contributions repository kutoka Github kwenda kwenye kompyuta yako.

Tengeneza branch:

Kwenye kompyuta yako, ukiwa kwenye terminal ingia kwenye repository uliyonakili

cd first-contributions

Sasa tengeneza branch kwa kutumia command ifuatayo git checkout command:

git checkout -b <add-your-new-branch-name>

Kwa mfano:

git checkout -b add-luke-oliff

(Jina la branch sio lazima lianze na neno add.)

Fanya mabadiliko na baada ya hapo commit:

Sasa fungua faili linaloitwa Contributors.md`, Andika jina lako. Usiweke jina lako mwanzoni au mwishoni mwa faili. Weka sehemu yoyote katikati. Baada ya hapo save faili.

git status

Ukiwa ndani ya directory hii kwenye terminal command ya git status itakuonesha mabadiliko yote uliyoyafanya.

Jumuisha mabadiliko yote uliyoyafanya kwenye branch uliyotengeneza kwa kutumia command git add command:

git add Contributors.md

Sasa commit mabadiliko uliyoyafanya kwa kutumia command ya git commit:

git commit -m "Add <jina> to Contributor list"

Badilisha neno <jina> na jina lako.

Tuma mabadiliko uliyoyafanya kwenda Github

Tuma mabadiliko uliyoyafanya kwa kutumia command ya git push:

git push origin <jina-la-branch>

Badilisha <jina-la-branch> na jina la branch ulilotengeneza hapo awali.

Kusanya mabadiliko uliyoyafanya kwa ajili ya uhakiki

Ukiwa Github kwenye repository hii utaona kitufe kilichoandikwa Compare & pull request. Bonyeza kitufe hicho.

create a pull request

Sasa tuma pull request.

submit pull request

Haitochukua muda mrefu nitaanza kuchukua mabadiliko yaliyofanyika na kuyapeleka kwenye master branch ya mradi huu. Utapokea email kukujulisha mara tu hatua hii itakapokamilika.

Nini cha kufanya baada ya hapa?

Hongera! umeweza kumaliza hatua za msingi ambazo ni fork -> clone -> edit -> PR ambazo utakutana nazo mara nyingi ukiwa kama mchangiaji!

Sheherekea hatua uliyofikia na wajulishe wengine kwa kwenda kwenye wavuti.

Waweza kujiunga kundi letu la slack endapo utakuwa unahitaji msaada wowote. Jiunge na kundi letu la slack.

Sasa tuanze kuchangia kwenye miradi mingine. Tumekusanya orodha ya miradi ambayo ina mambo mepesi unayoweza kuanza kushughulika nayo. Angalia Orodha ya miradi.

Mafundisho ya namna ya kutumia nyenzo nyingine

GitHub Desktop Visual Studio 2017 GitKraken VS Code Sourcetree App IntelliJ IDEA
GitHub Desktop Visual Studio 2017 GitKraken Visual Studio Code Atlassian Sourcetree IntelliJ IDEA